CHADEMA yazungumza kuhusu mgombea urais Zanzibar
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimedhamiria kusimamisha mgombea wa nafasi ya Urais Visiwani Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuwataka wanachama wenye nia ya dhati na nafasi hiyo, kuwasilisha barua zao ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Salum Mwalimu.

