TFF yaidhinisha kusimamishwa viongozi wa TEFA
Shirikisho la Soka Nchini TFF limekubaliana na uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) wa kuwasimamisha kwa muda wa miaka miwili viongozi watatu wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wilaya ya Temeke TEFA.

