Mabingwa watetezi wa La Liga mara ya mwisho kupoteza mchezo wa ligi ilikuwa miezi 13 iliyopita na imecheza michezo 42 bila kupoteza, Barca inashakilia rekodi za kutokupoteza kwenye michezo 43 ya ligi  iliyoanzia 2017 na 2018.Michezo mitatu iliyocheza Madrid dhidi ya Barcelona hivi karibuni  kikosi cha Carlo Ancelotti kimeshinda michezo yote.

25 Oct . 2024

Muda mrefu Tanzania tumekuwa kwenye kilio kupata waamuzi wenye ubora wa kuchezesha michuano mikubwa ya CAF. Sasa tumeanza kuona mwanga tunapaswa kuongeza juhudi ya kuandaa Waamuzi ambao watakuwa na ubora mkubwa kuanzia kwenye ligi yetu ya ndani ambao watatuletea heshima taifa letu.

25 Oct . 2024

Kocha mkuu wa Klabu ya Yanga Miguel Gamondi amesema ratiba ya Ligi Kuu ni ngumu kutokana na ukaribu wa michezo. Gamondi ameeleza hayo wakati mkutano na Waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Unioni hapo kesho Oktoba 26 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

25 Oct . 2024

Kevin Durant amefunga kwenye dakika za nyongeza na kuipa ushindi timu yake ya  Phoenix Suns wa Vikapu 116 dhidi ya  vikapu 113 vya Los Angeles Clippers usiku wa  Oktoba 23,  mchezo uliochezwa  uwanja wa Intuit Dome. 

24 Oct . 2024

Kocha wa Liverpool ya Uingereza Arne Slot raia wa Uholanzi  ameweka rekodi  ya Kuwa  Mkufunzi  wa kwanza kushinda michezo 11 kati ya 12 iliyocheza mwanzoni mwa msimu  na kuweke rekodi ya klabu hiyo

24 Oct . 2024

Klabu ya Namungo ya Ruangwa mkoani Lindi imemtangaza Juma Mgunda kuwa Kocha wao mkuu kuchukua nafasi ya Mwinyi Zahera ambaye amepangiwa majukumu mengine ndani ya klabu hiyo

24 Oct . 2024

Mfungaji bora wa muda wote wa NBA LeBron James usku wa jana Oktoba 22, 2024 aliweka rekodi nyingine  kwenye ligi ya kikapu Marekani maarufu NBA. King aliweka rekodi ya  kuchangia uwanja na mwanawe LeBron ‘Bronny’ James Jr mwenye umri wa miaka 20 kwenye mchezo uliozikutanisha  LA Lakers dhidi ya Minnesota TimberWolves  waliposhinda vikapu 110 kwa vikapu 103.

23 Oct . 2024

Nyota wa Real Madrid ya Hispania Vinicius Junior usiku wa jana Oktoba 22, 2024 aliushangaza ulimwengu wa Soka baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borrusia Dortmund uwanja wa Santiago Bernabeu. Vini alifunga magoli matatu na kuiongoza Madrid kupata ushindi wa goli 5-2.

23 Oct . 2024

Klabu ya Coastal Union ya Tanga  imemtangaza Juma Mwambusi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo baada ya kumfuta kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo David Ouma raia wa Kenya mwezi Agosti 2024. Kikosi hiko cha Wagosi wa Kaya kilikuwa chini ya Joseph Lazarao ambaye alikaimu kwa muda kipindi ambacho timu hiyo ilipokuwa inatafuta Mwalimu Mkuu.

23 Oct . 2024

Nahodha wa zamani wa Uruguay na Mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England atashiriki mashindano ya Tennis yatakayofanyika Uruguay Montevideo. Forlan ana umri wa miaka 45 atashirikiana na Federico Coria kwenye michezo ya wawili kwa wawili.

22 Oct . 2024

Aishi Manula mara ya mwisho kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania ilikua mwezi Machi 2024.Kumekua na mjadala mkubwa kwa Wapenzi na Wadau wa soka nchini Tanzania kuhusiana na nafasi ya Golikipa huyo wa timu ya Simba kwenye kikosi cha Stars. Manula hana Wakati mzuri kwenye klabu yake ya Simba ameondolewa kwenye nafasi yake ya kuwa golikipa namba moja baada ya kuumia kwa muda mrefu na aliporejea uwanjani kwenye mchezo wa Dabi ya Kariakoo alifanya makosa yaliyochangia kupoteza mchezo kwa goli 5-1.

22 Oct . 2024

Wachezaji wa timu za taifa za Wanawake zaidi ya 100 wameliandikia barua ya wazi Shirikisho la mpira Duniani FIFA kulitaka kuvunja mkataba wake wa udhamini na kampuni ya mafuta ya Saudi Arabia ya Aramco. Sababu kubwa zilizotajwa na Wachezaji hao ni kutokana na uharibifu wa Mazingira unaofanywa na kampuni hiyo ya uchimbaji wa mafuta, pamoja na uvunjwaji wa Haki za Binadamu nchini SaudI Arabia. Uwepo wa tamaduni ambazo zinamkandamiza Mwanamke nchini humo inatizamwa kama sababu kubwa zaidi ya Wachezaji wa timu za Wanawake kugomea mkataba huo wa udhamini. Aramco imesaini mkataba na FIFA utakaofika tamati mwaka 2027 ambapo kampuni hiyo itadhamini kombe la Dunia la Wanaume 2026 na Wanawake 2027.

21 Oct . 2024

Barani Ulaya kwa sasa Wachezaji Wanaongoza kwa ufungaji wa magoli kwenye ligi kuu Tano kubwa ni Washambuliaji wa kati. Mabadiliko ya Sayansi ya mpira wa miguu imepelekea kupoteza baadhi ya Wachezaji ambao walisifika kwa kutimiza majukumu yao yaliyokuwa yanawaweka ndani ya uwanja.Mabadiliko wa kiucheza na mifumo mipya kwenye mpira wa miguu imepelekea kuibuka kwa Wachezaji wa pembeni yao Mawinga kutumika kama Washambuliaji wa kati na kumfanya namba Tisa ili aweze kucheza awe na sifa ya kuchezesha wengine kama kiungo wa kutokea juu yaani inside Forward. Harry Kane, Karim Benzema na Robert Firmino ni mfano sahihi wa Washambuliaji wa kati wenye uwezo wa kuchezesha wengine ndani ya uwanja.

21 Oct . 2024

Moussa Camara Golikipa mpya raia wa Guinea alibeba matumaini makubwa ya Wana Msimbazi kwa kupata Mlinda Mlango ambaye anauwezo wa kucheza mpira kwa miguu yake. Katika michezo miwili mfululizo nyota huyo amefanya makosa ambaye yameigharimu klabu ya Simba alama 5 ambazo zinaweza kuwa alama muhimu kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu ambao timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi Karikaoo imeutafuta kwa misimu mitatu mfululizo bila mafanikio.

20 Oct . 2024

Harry Kane Mshambuliaji wa Bayern Munich jana alifunga goli tatu hat-trick dhidi ya Stuttgat na kufikisha idadi ya hat-trick Sita tangu ajiunge na Bavarians kutokea Tottenham Hotspurs ya Uingereza. Kane anashikilia rekodi ya kuwa Mchezaji mwenye asili ya Uingereza aliyefunga goli nyingi zaidi kwenye ligi kuu nchini Ujerumani mbele ya Kevin Keegan, Jude Bellingham na Tony Woodcock.

20 Oct . 2024