PNC ajuta kumpigia magoti Ostadh Juma na Musoma

Ijumaa , 30th Apr , 2021

Unakikumbuka kitendo cha msanii PNC kumpigia magoti Meneja Ostadh Juma na Musoma ili kumuomba kumrudisha katika lebo ya Mtanashati Entertiment, sasa msanii huyo amesema kitendo kile hakikukuwa serious ila anajutia kukifanya.

Picha ya PNC akimpigia magoti Ostadh Juma na Musoma

Akizungumzia suala hilo lililotokea mwaka 2014 kupitia show ya PlanetBongo ya East Africa Radio PNC amesema kuwa 

"Mimi na Ostadh Juma kuna vitu tulipishana na yeye hakupendezwa navyo, halafu mbali na muziki Ostadh alikuwa ananisaidia kama mdogo wake, ile picha ilikuwa ni utani sikuwa 'serious' kama ambavyo watu waliichukulia, nilikuja kuijutia ile picha baada ya maneno ya watu kuwa makubwa".

Tukio hilo lilisababisha msanii huyo kuongelewa zaidi na baadhi ya mashabiki na wadau wa muziki walilitafsiri kwamba kitendo hicho ni cha udhalilishaji