Jumanne , 1st Jul , 2025

Mkongwe wa timu ya Utah Jazz inayoshiriki ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA, Jordan Clarkson, ameachana rasmi na klabu hiyo, ambapo hivi sasa ni mchezaji huru na yuko kwenye makubaliano ya kujiunga na New York Knicks.

Clarkson mwenye umri wa miaka 33 ameitumikia Utah jazz kwa kipindi cha misimu sita, na hivi sasa Knicks wameonyesha nia ya kupata huduma yake kwa msimu ujao.

Timu ya Utah jazz inayotoka ukanda wa Magharibi ilikuwa na wakati mmbaya sana msimu huu baada ya kushika nafasi ya mwisho kwenye msimo wa ligi hiyo ikiwa imeshinda michezo 17 na kupoteza 65.