Tuesday , 8th Nov , 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Burundi linasema suala la urejeshwaji wa hiari kwa wakimbizi wa nchi hiyo linatarajiwa kupatiwa msukumo baada ya kuundwa kwa tume mpya itakayoratibu mchakato huo.

Wakimbizi wakisajiliwa katika kambi ya Kavumu

 

Mwakilishi mkazi wa UNHCR Burundi Abel Mbilinyi, amesema kuwa tume hiyo inatokana na ushauri wa Msaidizi wa Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Volker Turk aliyefanya ziara nchini Burundi juma moja lililopita.

Kadhalika Mbilinyi anaeleza namna tume hiyo itakavyoepuka mambo ya kisiasa na kujikita katika utendaji kwa kutumia weledi na pindi mambo yatakapokuwa juu ya uwezo wao wataishauri serikali yao kuchukua hatua stahiki.