Sunday , 29th Jun , 2025

Kiungo Fabrice Ngoma ameiaga Simba baada ya kuitumikia kwa miaka miwili. Ngoma ameishukuru Klabu hiyo kwa kuwataja Abdallah Salim Try Again na Mohamed Dewji Mo kwa kumleta nyota huyo msimbazi miaka miwili iliyopita.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Ngoma ameandika “Namshukuru kila mmoja ambaye alinifanya mimi kujisikia nipo nyumbani nikiwa Simba. Shukrani zangu ziende kwa Salim Abdallah ‘Try Again’ na Boss MO ambao walinileta mimi misimu miwili iliyopita. Shukrani kwa kocha, wafanyakazi na wachezaji ambapo kwa pamoja tulishirikiana katika chumba cha kubadilishia jezi.''

''Hatujaweza kuyafikia baadhi ya malengo yetu, lakini kumbukumbu zitasalia akilini mwangu na moyoni. Kwenu mashabiki wa Simba, ahsanteni kwa ushirikiano, msiiache hii timu, nyakati nzuri zinakuja hasa kwa kupitia kocha kama Fadlu. Ahsanteni na kila la kheri”