Alhamisi , 23rd Dec , 2021

Binadamu mrefu zaidi Duniani, Sultan Kosen (39) amesafiri kutoka Uturuki mpaka nchini Urusi kwa ajili ya kutafuta mke atakayemzalia mtoto.

Picha ya mtu mrefu zaidi duniani

Kosen anasema ameenda nchini Urusi kutafuta mke baada ya kusikia wanawake wa Urusi wanapenda wanaume wastaarabu na wamoto.

Kosen anashikilia rekodi ya Guinness ya mtu mrefu zaidi Duniani, anasema urefu wake muda mwingine unageuka kero na kumpa shida kwa sababu ya kuwa na mikono na miguu mirefu.

Mwaka 2013, Kosen alimuoa binti mrefu kutoka Syria, Merve Dibo aliyekuwa na urefu wa futi 5 na nchi 9 na kudumu miaka michache katika ndoa na kuachana kwa madai ya kwamba mawasiliano yao yalikuwa ya shida, yeye anaongea lugha ya Uturuki na mkewe alikuwa anaongea Kiarabu tu.