Carragher amesema licha ya uwezo mkubwa wa Salah, kuna hatari ya mastaa wakajiona muhimu kupita kiasi, jambo linaloweza kuathiri umoja wa timu.
"Mohamed Salah ni miongoni mwa wachezaji bora sana wa Liverpool, ila kuna tabia ya wachezaji wakubwa kujiona wao ndio kila kitu klabuni. Nataka kumkumbusha Salah na wakala wake kuwa kabla hajaja Liverpool, alikuwa anatambulika kama mchezaji aliyefeli Chelsea na hakuwa na kombe lolote," alisema Carragher.
Akaongeza kwa kusisitiza kuwa licha ya umaarufu wa Salah nchini kwao Misri, bado hajaleta mafanikio makubwa kimataifa:
"Yeye ni mchezaji mkubwa nchini kwao, lakini hana kombe lolote na timu ya taifa."
Kauli hiyo imeibua mijadala mitandaoni, hasa kufuatia taarifa za mvutano kati ya Salah na benchi la ufundi la Liverpool baada ya kuanzia benchi kwenye mechi dhidi ya West Ham.


