Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amefanya ziara ya kushtukiza kwenye bar iitwayo Barazani inayotiririsha maji machafu aina ya kinyesi cha binadamu na kumwamuru Mkuu wa wilaya ya Babati na OCD kuifunga bar hiyo mpaka mmiliki wake atakapojisalimisha mwenyewe ofisini kwake
Kitendo cha wananchi kukerwa na uchafu huo na kutosikilizwa na mamlaka za chini kimepelekea wananchi hao kupiga simu na kutoa kero yao kwa Mkuu huyo wa mkoa.
Awali Afisa Mazingira halmashauri ya mji Babati ameeleza kuwa mmiliki wa eneo hilo amekuwa akikaidi taarifa za afisa mazingira halmashauri ya mji za kutakiwa kufanya usafi mazingira hayo.



