Jumanne , 9th Dec , 2025

Rapa, producer na muigizaji wa Marekani 50 Cent amemtaja Diddy ni Adui/Mhalifu wake anayempenda zaidi.

Picha ya Diddy na 50 Cent

50 Cent ameongea hilo kwenye Interview aliyofanya baada ya kuulizwa kuhusu shujaa wake na mhalifu anayemkubali ambapo amemtaja Diddy.

Tayari 50 Cent ameachia Documentary ya 'Sean Combs: The Reckoning' inayohusu maisha ya Diddy, kufeli kwake, matukio yaliyomtokea na kesi zilizompeleka gerezani.

Zaidi ya miaka sasa 50 Cent na Diddy hawapikiki chungu kimoja,hawana uhusiano mzuri, chuki na utani wa kudhalilishana hadharani kati yao.