Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Miguna apigwa chini, Sonko afanya maamuzi

Wednesday , 13th Jun , 2018

Gavana wa Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi Mike Mbuvi Sonko amesema atachagua mgombea mwingine nafasi ya Naibu Gavana wa Nairobi baada ya bunge la kaunti ya Nairobi, Jumanne hii kukataa uteuzi wake wa Mwanasheria Miguna Miguna.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Sonko amesema atatoa jina jingine baada ya "ushauri wa kutosha."

"Nitawasilisha mteule mwingine aliyestahili kwenye bunge la kaunti ya Nairobi baada ya kushauriana kwa kuhakikisha kuwa Nairobi inapata Naibu  Gavana anayestahili kusaidia katika utoaji wa huduma," amesema Sonko.

Aidha ameeleza kwamba "Ninataka kukubali uamuzi wa bunge la kaunti ya Nairobi kukataa uteuzi wa Dk Miguna Miguna kama Naibu Gavana wa Nairobi kwa sababu ya uraia kama ilivyoelezwa kwenye  kifungu cha 78 cha Katiba."

Mbali na hayo Spika wa bunge Beatrice Elachi,  Jumanne hii  alielezea kwamba hakuwa na uwezo wa kujadili uteuzi wa Miguna kwa sababu afisa wa Serikali hawezi kushikilia uraia miwili.

Hata hivyo Serikali ya Kenya  imesisitiza mara kwa mara kwamba Miguna si raia wa Kenya, kwa hivyo, ataruhusiwa tu kuingia nchini humo kwa kutumia pasipoti yake ya halali ya Canada.

Katibu Mkuu wa Uhamiaji Gordon Kihalangwa alisema Miguna lazima aomba tena upya kurejesha uraia wake nchini Kenya.

Mei 17 mwaka huu Gavana Sonko alimpendekeza Mwanasheria Miguna kuwa Naibu Gavana wa Mji wa Nairobi.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja