Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga
Kufuatia hatua hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abrahaman Abdallah amesema kuwa awali katika kijiji hicho palikuwa na zahanati ambayo ilijengwa chini ya kiwango cha ubora hali iliyopelekea serikali kuifunga kwa muda mfupi kutokana na majengo yake kuchakaa hivyo kuwalazimu wananchi kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya.
Bw. Abrahaman Abdallah amehimiza kuharakishwa kwa ujenzi wa Zahanati unaoendelea kijijini humo ili changamoto hiyo iweze kumalizwa na kuondoa matatizo ya wananchi yanayowakanbili kwa sasa.
"Tayari shilingi milioni 28 zimetolewa na Zahanati imeshaanza kujengwa na ndani ya mwaka huu tutahakikisha inamalizika na kukamilika tayari kwa kuanza kutoa huduma, kwahiyo wakinamama wa Mwembeni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, ruksa kubeba mimba sasa" alisisitiza Mwenyekiti Rajab.
"Waliniambia wakinamama wa Mwembeni kwamba wamekubaliana na waume zao kwa muda sasa wasibebe ujauzito kwasababu wanapata shida inapofika wakati wa kujifungua kwakuwa wanakwenda mbali na muda lakini wakati mwingine wamekuwa wanajifungulia njiani hali inayohatarisha afya zao, " alisema Mwenyekiti huyo.