Sunday , 4th Nov , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda leo Novemba 4, 2018 amefanya sala maalum yenye lengo la kukemea maovu yanayoendelea ndani ya jiji la Dar Es Salaam.

Picha hii haihusiani na habari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akifanyiwa maombi.

Sala hiyo iliyofanyika Katika kanisa la Efatha jijini Dar Es Salaam, Mkuu huyo wa mkoa ametoa chozi mbele ya waumini wa kanisa hilo alipopewa nafasi ya kuongea juu ya mambo yanayoendelea katika mkoa wake.

RC Makonda amesema kuwa anauzunishwa na maovu yanayoendelea ndani ya jiji la Dar Es Salaam kwani kila kona kumejaa mateja, mashoga na kila aina ya uchafu jambo ambalo linahitaji nguvu kubwa kukemewa na kila mtu.

Akizungumza kanisani hapo, Makonda amesema "viongozi wengi tunabaki kusimamia vifungu vya sheria vilivypo kwenye vitabu na Katiba na kusahau kuwa kuna Mungu. Akiangalia katika mkoa wa Dar es salaam, namba moja  anamuona Makonda, anaona mashoga wamezagaa, madanguro na mateja wamejaa, unafikiri Mungu anaweza kuwa na furaha na mimi?".

"Sheria ipo lakini watu hawaiangalii, neno la Mungu halienei kama yanavyoenea madanguro na bar, watu wanao muda wa kufanya uzinzi lakini hawana muda wa kumwabudu Mungu", ameongeza Makonda huku akitoa machozi.

Sakata hilo lilianza Oktoba 31, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Paul Makonda alisema "leo zimefika ujumbe 18972 na hawa wote wanalaani na simu zilizokuwa zinapigwa ni nyingi sana niwasihi endeleeni kutuma ujumbe ili tuendelee kukomesha biashara hiyo haramu".