
Rais Samia Suluhu Hassan
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa wengine aliowateua ni Balozi Dkt. Jilly Elibariki Maleko, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). Balozi Maleko anachukua nafasi ya Balozi Begum Karim Taj ambaye amemaliza muda wake.
Aidha amemteua Prof. Eliakimu Mnkondo Zahabu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (National Carbon Monitoring Center - NCMC), pamoja na Lucas Abrahamani Mwino, ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), ambapo ameachukua nafasi ya Dkt. John Kedi Mduma ambaye amemaliza muda wake.