Jumatatu , 13th Mei , 2024

Zaidi ya nyumba tisa zilizopo mtaa wa barabara ya Mwinyi Kata ya Kiburugwa jimbo la Mbagala jijini Dar es salaam zimesombwa na yanayodaiwa kuwa maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua zizonaendelea kunyesha 

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Wakizungumza na EATV baadhi ya wananchi wakiwemo waathirika wa maafa hayo wamesema kwasasa hawana sehemu za kuishi wao na familia zao wakiwemo watoto huku baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na maeneo hayo wameingiwa hofu kuwa nyumba zao zipo hatarini pia kusombwa ambapo wanaishi kwa mashaka 

Mwenyekiti wa mtaa huo wa barabara ya Mwinyi Suleiman Malidiche amesema kubwa ambalo wanaliomba ni Serikali kuwawezesha wananchi walioathirika kupewa makazi na familia zao lakini wanaiomba pia Serikali kutuma wataalamu kujua nini hasa chanzo cha tatizo hilo 

Waathirika wa maafa hayo kwasasa wanaishi kwa majirani wao na watoto wao