Ijumaa , 10th Mei , 2024

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa, ameapa kula sahani moja na viongozi wa sekta ya afya wanaoshiriki kuzuia watumishi na watendaji kutopanda madaraja kwa sababu zao binafsi.  

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Waziri Mchengerwa ametishia kuwaondoa kwenye nafasi zao viongozi wote wanaohusika kukwamisha watumishi kupanda madaraja katika ngazi mbalimbali huku akisisitiza jambo la watumishi kupandishwa madaraja kuwa ndio kipaumbele chake. 

Mchengerwa ameyasema hayo wakati akifungua maadhimisho ya 51 ya siku ya Wauguzi yanayofanyika Kitaifa mkoani Tanga ambapo katika hotuba yake Rais wa chama cha wauguzi Tanzania Alexander Baluhya alisema mbele ya Waziri Mchengerwa kuwa jambo hilo limekuwa kilio chao cha muda mrefu sasa hususani kwa watumishi waliopo muda mrefu kazini.