Jumatano , 15th Mei , 2024

Baadhi ya vijana jijini Dar es Salaam wanojishughulisha na uokotaji wa makopo au chupa za plastiki zilizotumika wamesema chupa hizo ambazo huonekana wakiziokota mtaani kwa sasa wanauza shilingi 350 kwa kilo moja na wakati mwingine hufika hadi 400.

Chupa za plastiki

Wakizungumza na #EastAfricaTV wamesema kumekuwa na imani tofauti kuhusu watu wanaookota makopo wakidhaniwa kuwa ni wezi au watu wenye matatizo ya akili ambapo wamekunusha kauli hiyo kwa kusema wengi wao wanafanya kazi hiyo kama sehemu ya kupata kipato na kuendesha familia huku wengine wakitoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza na kuja Dar es Salaam kufanya shughuli hizo.