Jumanne , 14th Mei , 2024

Watu saba wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa mkoani Morogoro baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika eneo la Dakawa wilayani Mvomero.

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro SACP Alex Mkama amesema tukio hilo limehusisha gari aina ya Noah yenye namba za usajili T 101 DKB iliyokuwa inatokea Dumila kwenda Morogoro mjini kugongana na lori lenye namba za usajili RS 980 ambalo lilikuwa linatokea Morogoro kwenda Dodoma.

“Tukio hilo limetokea baada ya Lori kuacha njia yake baada ya kuover take na kukutana uso kwa uso na gari ya abiria Noah na kusababisha vifo na majeruhi kama nilivyosema”amesema Kamanda wa polisi Alex Mkama

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Mvomero Dkt. Frances Mogel amesema wamepokea majeruhi saba na miili ya watu waliofariki dunia ilikuwa sita

“Leo asubuhi tulikuwa tunatokea Dumila tumepanda Noah kufika bwawa la Hatari ndio Lori likatupush uso kwa uso,tulibahatika kutoka ndio kama unavyotuona ila wenzetu wengine wamefariki akiwemo na dereva wetu,amesema Maimuna Salum manusura wa aajali