Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo, wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Chiwanda wilayani humo.
Chongolo amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Momba Kenan Kihongosi, kuwatafuta na kuwachukulia hatua wale wote waliosababisha mimba hizo kwa watoto waliochini ya miaka 18 na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Hata hivyo ameagiza Mtendaji wa Kata ya Nkangamo na Mwenyekiti wa kijiji cha Chiwanda kutokubali kumaliza masuala hayo kienyeji, na watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwani wao ndio wanawatambua wananchi katika maeneo yao.