Ruud van Nistelrooy atakiongoza kikosi cha Mashetani Wekundu katika mchezo wa ligi siku ya kesho Jumatano dhidi ya Leicester City, huku klabu ikisubiri kumtambulisha Kocha mkuu muda wowote kuanzia siku ya kesho.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Simon Mdende,
Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 majina ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo yamekosekana kwenye orodha ya tuzo hizo. Zaidi ya miaka kumi na tano tuzo hizo zilitawaliwa na Wachezaji ambao wanatajwa kama Wachezaji bora wa muda wote kuwahi kutokea Duniani Messi na Ronaldo.
Pichani Ni Wakazi na Zuchu
Kocha wa klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno Ruben Amorim kwa mujibu wa vyombo vya Habari barani Ulaya vinamtaja kuwa ndiye kocha anayetizamiwa kuchukua nafasi ya Erik Ten Hag ndani ya Manchester United baada ya timu hiyo kutangaza kumfuta kazi Kocha huyo raia wa Uholanzi siku ya jana. Klabu ya Man United na Sporting Lisbon zipo kwenye majadiliano juu ya uhamisho wa Kocha huyo bora kwa sasa nchini Ureno.
Pichani Ni Zuchu na Lady Jaydee
Klabu ya Manchester United ya Uingereza imetangaza kumfuta kazi kocha wake Erik Ten Hag. Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Ten Hag amepata taarifa ya kufutwa kwake kazi asubuhi ya leo baada ya jana kupoteza mchezo wa ligi kuu Uingereza ugenini uwanja wa London Stadium nyumbani kwa timu ya West Ham United.
Nyota wa Golden State Warriors Stephen Curry amepata majeraha timu yake ikipoteza dhidi ya Los Angeles Clippers kwa alama 112-104. Curry alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi ya kikapu nchini Marekani maarufu NBA dhidi ya Clippers mchezo uliochezwa jana Jumapili Oktoba 27, uwanja wa Chase Center.