Jumanne , 2nd Dec , 2025

Mshambuliaji wa Ufaransa na Real Madrid, Kylian Mbappé, ameweka rekodi ya kuvutia baada ya kuwa mchezaji wa nne katika karne ya 21 kufunga magoli 60 au zaidi ndani ya mwaka mmoja (kwa klabu na timu ya taifa).

 

Kwa mafanikio hayo, Mbappé sasa anajumuishwa na magwiji Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Robert Lewandowski, waliowahi kuifikia au kupita idadi hiyo ya mabao katika mwaka mmoja.

Mbappé bado ana mechi kadhaa kabla ya mwaka kuisha, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza idadi hiyo na kujiweka kwenye nafasi ya kipekee zaidi.

Wachezaji waliowahi kufunga 60+ mabao ndani ya mwaka mmoja (karne ya 21):
- Lionel Messi – 91 mabao (2012)  
- Cristiano Ronaldo – 60 mabao (2011)  
- Cristiano Ronaldo – 63 mabao (2013)  
- Robert Lewandowski – 69 mabao (2021)  
- Kylian Mbappé – 60+ mabao (2025)