Wednesday , 3rd Dec , 2025

Lord Swire ameiomba Tanzania kuwa mshirika wa kimkakati ili kuchochea wawekezaji wengi kutoka washirika wa Jumuiya hiyo ya Madola. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Mhe. Lord Hugo Swire, Ikulu Jijini Dar es Salaam jana tarehe 02 Desemba, 2025.

Rais Dkt. Samia pamoja na Naibu Mwenyekiti wa CWEIC Lord Hugo Swire ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani Mambo ya Nje wa ofisi ya Jumuiya ya Madola katika Serikali ya Uingereza walijadiliana masuala ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji ambao utachochea ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira nchini.

Kwa upande wake Lord Swire ameiomba Tanzania kuwa mshirika wa kimkakati ili kuchochea wawekezaji wengi kutoka washirika wa Jumuiya hiyo ya Madola.