Jumatatu , 11th Apr , 2022

Mganga mmoja wa tiba za kienyeji katika Wilaya ya Itilima mkoani amejitolea kwa gharama zake kujenga vyumba viwili vya madarasa ya kisasa, kuchimba kisima cha maji na kuweka umeme wa Sola kwenye shule mbalimbali wilayani humo,

Mganga wa tiba za kienyeji katika Wilaya ya Itilima mkoani Ndabagija Katani

Mganga huyo Ndabagija Katani amesema ameamua kufanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua maendeleo ya elimu.

Katika mahojiano yake na Runinga ya East Africa, Mganga huyo amesema suala la kuchangia maendeleo halipaswi kuachwa kwa Serikali pekee, bali kwa kila Mtanzania.

Ndabagija ambaye ni mkazi wa kata ya Chinamili Wilaya ya Itilima, amewashauri waganga wengine wa kienyeji nchini, kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo ya Taifa.