Wednesday , 3rd Dec , 2025

“Unajua hatari tunayokabiliana nayo kutoka kwa vyombo vya usalama, kwa sababu hiyo nimeamua kuvaa koti la kuzuia risasi. Wenzangu wengi wamekuwa na wasiwasi na tumepata taarifa kwamba ninaweza kulengwa. Sijisikii salama kwa sababu ya koti hili lakini tunajaribu kufanya tuwezavyo"

Mgombea urais wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu Bobi Wine amesema kuwa ameamua kuvaa koti la kuzuia risasi maisha yake yako hatarini.

Kauli hiyo ya Bobi Wine imekuja baada ya timu yake kupambana na vikosi vya usalama matumizi ya risasi, mabomu ya machozi na kukamatwa kwa wafuasi wake kukishuhudiwa nchini humo.

Bobi Wine anavishutumu vikosi vya usalama kwa kuingilia kampeni zake kwa kuziba barabara na kuwakamata wafuasi wake huku vyombo vya usalama vikisisitiza kuwa Bobi Wine hafuati miongozo na kwamba wafuasi wake wamewashambulia kwa kutumia mawe. Sasa Bobi Wine ameamua kuanza kuvaa koti la kuzuia risasi.

“Unajua hatari tunayokabiliana nayo kutoka kwa vyombo vya usalama, kwa sababu hiyo nimeamua kuvaa koti la kuzuia risasi. Wenzangu wengi wamekuwa na wasiwasi na tumepata taarifa kwamba ninaweza kulengwa. Sijisikii salama kwa sababu ya koti hili lakini tunajaribu kufanya tuwezavyo kuzuia hatari lakini kwa ujumla tunajua Mungu ndiye mwenye nguvu zaidi” amesema.

Vikosi vya usalama vimedai yeye na wafuasi wake wamekuwa wakikiuka miongozo ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 mwezi January 2026.