Jumatano , 3rd Dec , 2025

Hukumu hiyo ya kesi namba 10468/2025 imesomwa Desemba 01, 2025 na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Fredrick Shayo baada ya upande wa Mashtaka kuthibitisha kutendwa kwa kosa hilo mnamo Februari 03, 2025 katika maeneo ya barabara ya Halmashauri ya Mlandizi, Kibaha

Mohamed Juma Mohamed maarufu kama Mudy Mweusi (23) ambaye ni dereva bodaboda na mkazi wa Mtongani Mlandizi na Ashrafu Adam Kida maarufu kama Shila (19) ambaye ni fundi makenika na mkazi wa Kidile, Mlandizi wamehukumiwa kifungo cha maisha jela na kulipa fidia kiasi cha shilingi milioni 10 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka kwa pamoja binti wa miaka 18.

Hukumu hiyo ya kesi namba 10468/2025 imesomwa Desemba 01, 2025 na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Fredrick Shayo baada ya upande wa Mashtaka kuthibitisha kutendwa kwa kosa hilo mnamo Februari 03, 2025 katika maeneo ya barabara ya Halmashauri ya Mlandizi, Wilaya ya Kibaha.

Imeelezwa kuwa, kabla ya tukio hilo binti huyo alikodi pikipiki kutoka Mlandizi kuelekea Ruvu Stesheni ndipo akiwa njiani dereva alisimamisha pikipiki kisha wenzake wawili ambao aliounga nao njama walifika eneo hilo na kuanza kumbaka binti huyo.

Shayo ameeleza kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130 (1), 131 (1) na 131 A (1) na (2) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.