Bilal ataka udhibiti wa silaha haramu
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal amezitaka nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika, kuhakikisha wanatafuta suluhisho la kudhibiti kuzagaa kwa silaha haramu ndogondogo, zinazovunja amani katika nchi nyingi barani Afrika.

