Makamu wa rais wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal.
Dkt. Bilal amesema hayo leo Jijini Dar-es-Salaam wakati akifungua mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani kutoka nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika wenye kukipa nguvu zaidi chombo kitakachofanya kazi ya kuzuia na kuzagaa kwa silaha ndogo ndogo katika nchi hizo kinachojulikana kama Regional Centre For Small Arms (RECSA).
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Pereira Silima ametolea mfano wa Jiji la Dar es Salaam kwamba limekuwa na matukio ya mara kwa mara yanayohusisha silaha ndogo ndogo jambo ambalo amesema bado linahitaji udhibiti ili zisiendelee kuathiri maisha ya wananchi ama kuwajeruhi.

