Vijana wawili wa Copa Coca Cola kwenda Brazil
Vijana wawili zao la kopa Cocacola, Ally Mabuyu kutoka jijini Dar Es Salaam na Juma Yusuph kutoka Zanzibar wamebahatika kupata nafasi ya kwenda nchini Brazil kushuhudia ufunguzi wa kombe la dunia. Wakiongea mbele ya waandishi wa habari mara tu baada ya kutambulishwa, vijana hao wamesema huo ni mwanzo wa kutimia ndoto zao za kufanikiwa katika soka na kuchezea timu ya taifa.