NHIF yafikiria kutoa bima ya afya kwa walemavu
Mfuko wa Bima ya Afya nchini Tanzania umesema changamoto inayoukabili mfuko huo hivi sasa ni jinsi ya kuhakikisha inatoa huduma hiyo kwa kundi la watu wasio na uwezo pamoja na wale wenye mahitaji maalumu wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu.

