Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Marehemu Nasra Mvungi katika uwanja wa jamhuri Morogoro, muda mfupi kabla ya maziko.
Hatimaye mwili wa mtoto Nasra Mvungi aliyefariki dunia katika hospitali ya taifa ya Muhimbili umeagwa rasmi katika uwanja wa Jamhuri na kuzikwa katika makaburi ya Kola manispaa ya Morogoro.