AU lawamani sakata la utekaji watoto Nigeria
Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayojishughulisha na haki za wanawake na watoto nchini Tanzania, yameutaka umoja wa Afrika kuingilia kati kuwezesha kuachiwa kwa wanafunzi zaidi ya 200 waliotekwa nchini Nigeria na kikundi cha Boko Haram.