Msuya apiga marufuku wafanyabiashara wa vyakula
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Aziz Msuya amesema wanatarajia kuanza kutumia nguvu kukataza wafanyabiashara wa chakula wanaofanya biashara zao katika maeneo yaliyoathirika na kipindupindu kutokana na ongezeko la wagonjwa wa kipindupindu.

