Serikali yapongezwa marufuku ya Shisha
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku Tanzania, Bi. Lutgard Kagaruki, amepongeza serikali kwa kupiga marufuku uvutaji holela wa sigara pamoja na kukataza matumizi ya shisha iliyokua inaangamiza afya za vijana wengi Tanzania.
