Serikali kukusanya bilioni 200 kiwanda cha Nondo
Serikali ya Tanzania inatarajia kukusanya sh. bilioni 200 kwa mwaka, ikiwa ni mapato ya kodi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha kimataifa cha Kiluwa Steel Group, kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha tani 3,000 za nondo kwa siku.
