Meneja kitengo kikuu cha utabiri kutoka mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA Bw. Samwel Mbuya.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za vuli zinazoendelea kunyesha nchini ni mvua ambazo kama wananchi hawatachukua tahadhari za haraka zinaweza kuleta madhara makubwa.