Walioghushi vyeti kupata mikopo kutinga mahakamani
Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa baada ya uhakiki wa vyeti vya vifo vilivyowasilishwa na wanafunzi wanaoomba mikopo wakidai kwamba ni yatima, watakaobainika kupeleka vyeti vilivyoghushiwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.