Ndalichako apiga marufuku matumizi holela ya joho
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amepiga marufuku matumizi ya vazi aina ya ‘Joho’ kwenye sherehe za mahafali ya ngazi za chini za elimu na kutaka litumike kuanzia ngazi ya Shahada ili kulipa heshima vazi hilo.