Wachezaji wapya Azam FC kupimwa ubavu kwa Mtibwa
Katika kujiandaa na mechi za raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Azam FC, inatarajia kukipima kikosi chake kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Jumamosi Desemba 10 saa 1.00 usiku.
