Watu 5 wachomwa visu mwilini, wawili wafariki
Watu wawili wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa, baada ya kuchomwa kwa kisu sehemu mbalimbali za miili yao, huku mmoja anayedaiwa kuwawachoma visu watu hao, akidaiwa kupigwa na wananchi, katika kituo kikuu cha mabasi manispaa ya Bukoba.