Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa Rais, Ubunge na Madiwani majimbo la Uyole na Mbeya Mjini mkoani Mbeya Anamary Joseph amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kupanga na kuweka taarifa zao katika bahasha zilizowekwa ili kuepusha mkanganyiko.
Wito huo umetolewa leo katika ukumbi wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia MUST kabla ya kuwaapisha wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kutoka majimbo ya Uyole na Mbeya Mjini huku akiwataka kuwa makini kupanga na kuweka taarifa katika bahasha zilizopangwa.
Wasimamizi wa uchaguzi nao wamesema kuwa wanameshajipanga kufanya kazi kwa utaratibu na sheria zilizowekwa ili kulifanya zoezi hilo kwa ukamilifu ili kuepusha migogoro wakati wa zaozi nzima la uchaguzi mkuu ambao utafanyika Oktoba 29,2025.

