
Trump aliitoa kauli hiyo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Zelensky akipendekeza uwepo wa mpango wa usitishwaji mapigano katika maeneo ya mstari wa mbele wa vita na kumtaka Zelensky kukubali kuyaachia maeneo yaliyonyakuliwa na Urusi, wazo linalopingwa vikali na Zelensky
Vyanzo kadhaa vimesema Trump huenda alishawishiwa na Putin wakati walipozungumza kwa njia ya simu siku ya Alhamisi ambapo kulingana na gazeti la The Washington Post, Putin alipendekeza Ukraine kuiachia mikoa ya Donetsk na Luhansk na kusalia sehemu ndogo ya Zaporizhzhia na Kherson.
Trump alitangaza pia kusitisha azma ya kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu ya Tomahawks akisema kuwa nchi yake pia inayahitaji:
Aidha Trump, amesema atasimamia makubaliano hayo kwa kutoa hakikisho la usalama kwa pande zote, kauli iliyowachukiza maafisa wa Ukraine waliohudhuria mkutano huo wa Ijumaa.
Kwa upande wake Zelensky amemuomba Trump kumshinikiza zaidi Putin kumaliza vita akisisitiza kuwa Urusi ina nguvu kuliko kundi la Hamas, hivyo itakuwa vigumu kufikia makubaliano ya amani huku rais huyo wa Marekani akimsisitizia Zelensky kwamba Putin ametishia kuiharibu Ukraine ikiwa haitatii masharti hayo.