Jumapili , 26th Oct , 2025

Mara baada ya kuwasili nchini humo, Majaliwa amepata fursa ya kuzungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya anaeiwakilisha Tanzania nchini Sychelles Dkt. Bernard Kibesse.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili nchini Seychelles kwa ajili ya kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais mteule wa nchi hiyo Dr. Patrick Herminie.

Waziri Mkuu Majaliwa amepokelewa katika uwanja wa ndege wa visiwa hivyo na Balozi wa Heshima Maryvonne Pool, Balozi wa Seychelles Selby Pillay na Balozi wa Tanzania nchini Kenya anaeiwakilisha Tanzania nchini Sychelles Dkt. Bernard Kibesse, leo Oktoba 26 2025.

Mara baada ya kuwasili nchini humo, Majaliwa amepata fursa ya kuzungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya anaeiwakilisha Tanzania nchini Sychelles Dkt. Bernard Kibesse alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sychelles kumuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye uapisho wa Rais mteule wa nchi hiyo Dr. Patrick Herminie.

Wengine waliokuwepo katika mazungumzo hayo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Cosato Chumi, Balozi wa Heshima Maryvonne Pool na Balozi wa Seychelles Selby.

Patrick Herminie, Kiongozi wa upinzani nchini Shelisheli, alishinda kinyang'anyiro cha urais nchini humo, akimshinda kiongozi aliyekuwa madarakani Wavel Ramkalawan katika duru ya pili ya kura, kulingana na tume ya uchaguzi katika uchaguzi uliofanyika mapema mwezi Oktoba.

Herminie alishinda asilimia 52.7 ya kura, huku Ramkalawan akipata asilimia 47.3, matokeo rasmi yaliyotangazwa mapema Jumapili iliyopita yalionyesha.