Jumatatu , 20th Oct , 2025

Ndege ya mizigo imeteleza kutoka kwenye njia ya kurukia ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong na kutumbukia baharini na kuua watu wawili, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Ndege ya Emirates EK9788, inayofanya kazi ya kusafirisha mizigo, ilikuwa ikiwasili kutoka Dubai mwendo wa saa kumi kasoro dakika kumi saa za ndani (19:50 GMT) ilipogonga gari kwenye barabara ya kaskazini.

Wafanyakazi wawili wa uwanja wa ndege walianguka baharini, taarifa kutoka kwa idara ya Usafiri wa Anga inasema.
Waliokolewa lakini baadaye walikufa hospitalini, kulingana na vyombo vya habari vya ndani ikiwa ni pamoja na shirika la utangazaji la RTHK ambalo lilinukuu taarifa ya polisi.

Ndege hiyo ilianguka kwenye uzio wa uwanja wa ndege na kugongana na gari la polisi waliokuwa wakishika doria kando ya njia ya ndege kurikia na kulisukuma gari hilo hadi likatumbukia baharini.

Wafanyakazi wawili wa usalama waliokuwa kwenye gari hilo, wenye umri wa miaka 30 na 41, walifariki kutokana na tukio hilo