Jumla ya Makarani waongozaji 422 wa usimimizi wa Uchaguzi Mkuu katika majimbo mawili ya Bunda na Jimbo la Mwibara wameapishwa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la uchaguzi la Bunda na Mwibara Oscar Nchemwa amesema makarani hao wanapaswa kusoma na kufuata kanuni na Sheria za uchaguzi ili kuepuka migongano ya kisiasa wakati wa upigaji kura na kuzua taharuki zisizo na lazima na kuharibu mchakato wa Uchaguzi.

