Shaa kuungana na wakali Afrika
Msanii wa kike nchini Tanzania Shaa ambaye hivi sasa amefyatua wimbo wake mpya 'Subira' ataungana na wasanii mbalimbali kutoka barani Afrika katika kutengeneza muziki wenye mchanganyiko wa vionjo vya kisasa vyenye asili ya Afrika.

