Penzi lanoga kwa Witnesz na Ochu, watarajia mtoto
Rapa mkali wa Kike, Witnesz ambaye kwa sasa ni mjamzito mwenye matarajio ya kuwa mama ndani ya miezi kadhaa ijayo, kupitia eNewz rasmi, ameweka wazi juu ya mahusiano yake na msanii Ochu Sheggy ambaye pia kwa sasa muda wote wanafanya muziki pamoja.