Bunge lapiga kalenda Muswada wa misamaha ya kodi.
Kamati ya bunge ya Bajeti imekataa kubariki Muswada wa Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani VAT na Muswada wa Sheria ya utawala wa kodi ambao ulikuwa uwasilishwe bungeni jumatatu ijayo na kujadiliwa ili misamaha ya kodi isiyo na tija ifutwe.

