Tanzania ina uhaba wa wataalamu tiba ya usingizi
Zaidi ya wagonjwa milioni mbili wanaopaswa kupewa dawa za usingizi na maumivu, hususani wale wanaofanyiwa upasuaji nchini Tanzania wapo katika hatari ya kukosa huduma hiyo kwa ubora, kutokana na uhaba wa wataalam wa kutoa dawa za usingizi na maumivu.