Mboto Haji
Mboto amesema kuwa, anapendana sana na mpenzi wake huyu isipokuwa katika swala la kuoa, bado ni mapema kufanya hivyo kutokana na imani yake kuwa mambo haya hayahitaji haraka.
Pembeni ya ishu ya maisha binafsi ya Mboto, Msanii huyu pia amegusia kuwa na kazi mpya na kubwa ya filamu ambayo ameifanya na Marehemu Rachel Haule aliyefariki hivi karibuni, ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni kati ya kazi nyingine kali.







